KATIBU MKUU WA DIVISHENI YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI WA KANISA LA WAADIVENTISTA WASABATO AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA KANISA LA WASABATO KIGAMBONI IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA EXTRA VAGANZA YANAYOFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM, KATIKA UWANJA WA TAIFA.
Moja ya Mashemasi wa Kiume wa Kanisa la Kigamboni akiwa katika jiwe la Msingi kabla ya uzinduzi
Katibu Mkuu wa Unioni ya Kaskazini mwa
Tanzania, Mchungaji Davis Fue, akiangalia ramani ya jengo la kanisa la
Waadventista Wasabato litakavyokuwa mara baada ya kumalizika, wakati wa uwekaji
jiwe la msingi la kanisa hilo jana mchana, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya
Extra Vaganza, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na
kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba, (wa nne
kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa
la Wasabato kigamboni, wazee wa kanisa hilo na baadhi ya washiriki wa kanisa
hilo, jana mchana mara baada ya kuweka jiwe la msingi. Wa nne kutoka kulia ni
Katibu wa Union ya Kusini Mwa Tanzania, Mchungaji James Machage.
Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na
kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba, akifungua
kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la kanisa la Waadiventista Wasabato
Kigamboni jana mchana, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya extra vaganza yanayoendelea
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment